Wikimedia Research/Design Research/Research Participant Program/sw

अन्य भाषाएँ: Bahasa Indonesia • ‎Deutsch • ‎English • ‎Türkçe • ‎español • ‎français • ‎português • Kiswahili • ‎русский‎українська • ‎العربية • ‎فارسی‎हिन्दीবাংলা • ‎‎தமிழ் • ‎ไทย • ‎中文日本語 • ‎

Kushiriki katika Utafiti wa Wakfu wa Wikimedia edit

Katika Wakfu wa Wikimedia, tumejitolea kuboresha Wikipedia na miradi mingine ya Wikimedia iweze kutumika na kufikiwa kwa urahisi, kwa watu wengi iwezekanavyo. Utafiti kamili na thabiti juu ya mahitaji na uzoefu wa watumiaji wetu wa sasa na wa baadaye hutusaidia kuhakikisha kuwa muundo wetu wa bidhaa unaweza kuafikia lengo hili. Hii ndiyo sababu tunategemea mitazamo anuwai katika utafiti wetu. Tunatambua kuwa kuna vizuizi vya kushiriki katika utafiti wetu kwa wengine, na tunathamini wakati, juhudi, na maarifa ambayo watu hawa wanatoa kwa mchakato wa utafiti. Kwa kuzingatia desturi bora za utafiti, kupunguza vizuizi vya ushiriki na kufidia wakati na gharama ya intaneti iliyotumiwa, tumejitolea kutoa bahashishi kwa washiriki wetu.

Kufuzu kwa Utafiti wenye Bahashishi edit

Washiriki wa utafiti husajiliwa moja kwa moja kutoka kwa akiba yetu na jamii ya watumiaji wa Wikimedia. Sisi hutafuta watumiaji walio na sifa mahususi kama vile shughuli za watumiaji, aina ya mtumiaji, lugha za asili, jukumu katika mradi wa Wiki, ushirika wa jamii, vifaa vinavyotumika kusoma au kuhariri, n.k. Kuna njia kadhaa tunazotumia kupata washiriki wa utafiti ambao wataafikia vigezo vya utafiti. Ili kupata aina sahihi za washiriki, tunaweza kuomba mapendekezo kwa uhusiano wa jamii, kuwasiliana na wahariri kwenye Kurasa zao za Mazungumzo, au kutuma ujumbe wa usajili kwenye Ukurasa wa Majadiliano ya Kiufundi na Sera au ukurasa kama huo. Mara nyingi tunawaomba watumiaji wanaopenda kuwasilisha uchunguzi ili kuhakikisha kuwa mtumiaji anatimiza mahitaji ya utafiti mahususi. Tutatuma pia taarifa ya faragha inayoelezea jinsi Wakfu wa Wikimedia unavyopanga kutumia na kuhifadhi maelezo ya kibinafsi ambayo washiriki hutoa katika utafiti wa uchunguzi na wakati wa kikao cha utafiti. Timu yetu itawasiliana na watumiaji waliohitimu kuwaarifu juu ya kushiriki kwenye utafiti, pamoja na habari juu ya bahashishi inayotolewa kwa kushiriki. Kwa wale waliochaguliwa kushiriki, tutatuma pia fomu ya idhini kwa washiriki kutia saini inayoelezea shughuli za utafiti na kutoa ruhusa iliyo na kikomo kwa WMF kwa matumizi ya data na maarifa yaliyopatikana kwenye kikao. Baada ya shughuli za utafiti kukamilika, timu ya utafiti itatoa bahashishi kwa mshiriki.

Timu yetu mara nyingi huwapa mikataba washirika wa utafiti wanaoishi na walengwa. Washirika hawa “wengine” wa utafiti wanaweza kuhusika katika hatua yoyote ya utafiti ilivyoelezwa hapo juu. Wote wamesaini makubaliano ya kuweka siri, yaani wamekatazwa kutoa maelezo au data ya watumiaji nje ya mradi waliopewa kandarasi. Washirika wa utafiti wanaweza kuwasiliana na washiriki, kufanya vikao vya utafiti, na wanaweza pia kulipa bahashishi.

Shughuli Zisitolewa Bahashishi edit

Bahashishi au fidia hutolewa tu wakati imebainishwa wazi na timu ya utafiti wakati wa usajili. Shughuli zinazostahiki bahashishi huanza tu baada ya utafiti wowote unaofaa wa uchunguzi na baada ya kukamilisha shughuli zilizoratibiwa. Hatutoi bahashishi au fidia kwa mazungumzo mengine yoyote au shughuli ambazo hazijaelezewa hapo juu. Mifano ya shughuli ambazo hazipewi fidia ni mawasiliano ya barua pepe au mawasiliano ya mitandao ya kijamii, tafiti isipokuwa iwapo imedhihirishwa kutolewa bahashishi, maoni au maelezo juu ya huduma au mipango nje ya kikao cha utafiti, tafiti za uchunguzi, n.k.

Ugawaji wa Bahashishi edit

Timu yetu ya utafiti itafanya kazi na washiriki kuamua usambazaji wa bahashishi kabla ya shughuli za utafiti kuanza. Kukubali bahashishi ni kwa hiari na washiriki pia wana fursa ya kutoa bahashishi yao kwa kitengo cha Wikimedia au shirika lisilo la faida ikiwa wangependa.

Kiasi cha bahashishi huamuliwa kwa kila mradi na timu ya utafiti kulingana na mahitaji ya utafiti. Kwa miradi mingine tunatoa kiwango sawa, bila kuzingatia anakotoka mshiriki. Kwa miradi mingine, tunatoa kiwango kulingana na eneo. Tunaanza kwa kiwango cha msingi cha gharama ya maisha kulingana na wanakotoka washiriki. Tunabadilisha kiwango hiki kulingana na muda wa kikao cha utafiti, ujuzi wowote maalum unaohitajika, na data ya intaneti inayotumika wakati wa kikao. Wakati wowote inapowezekana, tunashauriana na washirika katika maeneo watokako washirika kutusaidia kutuarifu juu ya viwango vya kawaida.

Kwa wakati huu, tunaweza tu kutoa misaada kupitia huduma zifuatazo: Ethn.io, Tremendous.com, na Paypal.com. Masharti ya huduma kwa kampuni hizi yamechapishwa kwenye tovuti zao, na kukubali bahashishi kunaashiria kuwa mshiriki anakubali masharti yote. Kwa sababu ya vikwazo vya kufikia huduma hizi, hatuwezi kutoa bahashishi kwa wale walio nje ya maeneo yanayoshiriki, ingawa tunaendelea kushughulika ili kusuluhisha tatizo hili. Wakati mwingine, Paypal inaweza kuwa huduma pekee inayofanya kazi katika nchi fulani. Ikiwa hivyo, mshiriki atalazimika kupokea malipo kupitia Paypal ambayo itahitaji akaunti ya Paypal.

Shiriki edit

Ikiwa ungependa kuwa katika kikosi cha washiriki wetu wa utafiti, tafadhali jiandikishe hapa. Tunaweza kuwasiliana nawe mara kwa mara kuhusu fursa za kushiriki katika miradi yetu ya utafiti. Tafadhali tazama taarifa yetu ya faragha. Unaweza kujiondoa kwenye kikosi cha washiriki wakati wowote kwa kuwasilisha fomu hii.

Jinsi ya Kuwasiliana edit

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu mpango wetu wa utafiti wenye bahashishi, tafadhali wasiliana na desresadmin@wikimedia.org.