Ukuaji/Majarida/28

This page is a translated version of the page Growth/Newsletters/28 and the translation is 96% complete.

Jarida la timu ya Ukuaji #28

 

Karibu kwenye jarida la ishirini na nane kutoka kwa Timu ya Ukuaji! Saidia kutafsiri

 
Mpangilio wa Jumuiya, dhana A: Mtindo wa Accordion
 
Mpangilio wa Jumuiya, dhana B: Mtindo wa Dashibodi

Mpangilio wa Jumuiya 2.0

  • Mpangilio wa Jumuiya 2.0 ni kipengele kitakachowezesha jumuiya za Wikimedia kubinafsisha kwa urahisi na kupangilia vipengele ili kukidhi mahitaji yao ya kipekee. Mbinu hii huwapa wasimamizi wasio wa kiufundi uhuru zaidi na udhibiti wa kuwezesha/kuzima na kubinafsisha vipengele vya jumuiya zao.
  • Mbinu ya kiufundi na kazi zinazohusiana zimefafanuliwa katika jukumu hili la kubwa kwenye Phabricator.
  • Miundo ya awali imeandaliwa kwa mbinu mbili tofauti (tazama picha). Hivi karibuni tutaonesha mifano wasilianifu kwa wakabidhi wanaovutiwa, wasimamizi, na wahariri wenye uzoefu (T346109). Tafadhali tujulishe ikiwa una maoni kuhusu usanifu wa muundo, au ungependa kushiriki katika majaribio ya mfano.

Ufunikaji wa anwani za IP

  • Timu ya Ukuaji imekuwa ikifanya kazi katika masasisho kadhaa ili kuhakikisha vipengele vinavyodumishwa vya Ukuaji vitaendana mahitaji ya hapo baadaye Mabadiliko ya ufunikaji wa anwaniza IP. Kazi hii imejumuisha mabadiliko ya msimbo hadi: Mabadiliko ya Hivi Karibuni (T343322), arifa za Echo (T333531), kiendelezi cha Shukrani (T345679) na Ushauri (T341390).
  • Kabla ya Desemba, Timu ya Ukuaji itaanzisha majadiliano ya jumuiya kwa lengo la kuhamisha jumuiya kutoka mtiririko hadi Nyenzo za mijadala. Hatua hii inalenga kupunguza hitaji la kazi ya ziada ya uhandisi ili kufanya mitiririko iendane na Ufunikaji wa anwani za IP. (T346108)

Ushauri

Kukuza vipengele vya ukuaji

  • Tunaendeleza uwekaji wa kazi zilizopangwa "ongeza kiungo" kwenye Wikipedia zote. Tunapanga kuongeza kazi kwa Wikipedia zote ambazo zina mapendekezo ya viungo yanayopatikana kufikia mwisho wa 2023.
  • Tunapanga kuongeza Moduli mpya ya Athari kwenye Wikipedia zote hivi karibuni, lakini kwanza tunachunguza hitilafu kwa kazi inayoonyesha upya data ya Moduli ya Athari. (T344428)
  • Katika baadhi ya wiki, wageni wanaweza kufikia kazi iliyoandaliwa ya "kuongeza picha". Jukumu hili linapendekeza picha ambazo zinaweza kuwa muhimu kuongeza kwenye makala ambayo hayajaonyeshwa. Wageni katika wiki hizi sasa wanaweza kuongeza picha kwenye sehemu za makala ambazo hazijaonyeshwa. (T345940) Wiki zilizo na jukumu hili zimeorodheshwa chini ya "Mapendekezo ya Picha" kwenye jedwali la uwekaji la Timu ya Ukuaji.

Habari nyingine

  • We disabled the “add an image” task temporarily (T345188) because there was a failure in the image suggestions pipeline (T345141). This is now fixed.
  • Unaweza kusoma ripoti ya kuhusu uwakilishi wa Timu ya Ukuaji kwenye mkutano wa Wikimania huko Singapore hapa. Wajumbe wa Timu ya Ukuaji waliwasilisha vikao viwili wakati wa mkutano wa Wikimania Singapore.
  • Baada ya ushirikiano wa miaka 2.5 na Wikipedia ya Bangala, tumeamua kuanza ushirikiano na wiki nyingine. Wikipedia ya Kiswahili sasa ni mradi wa Wiki wa Majaribio kwa ajili ya majaribio ya Ukuaji.

Jarida la Timu ya Ukuaji lililotayarishwa na Timu ya Ukuaji na kuchapishwa na botToa maoni Jisajili au ujiondoe.